KATIKA hali isiyotarajiwa katika
wasanii wanaounda kundi la Bongo movie wamejikuta wakijitenga kushiriki
msiba wa Baba mzazi wa msanii mwenzao Wema Isack Sepetu, baada ya
kuundwa zengwe na mmoja wa watu wenye ushawishi katika kundi hilo, Wema
akiongea
kwa uzuni amesema kuwa hata wale waliofika jana katika msiba
huo hawakufika kwa ajili ya kumfariji bali walifika kwa ajili ya
kumsanifu.
FC ilifanya utafiti ili kubaini hilo
kwa kuwapigia simu baadhi ya wasanii wanaotoka katika kundi hilo nao
bila kusita kwa masharti ya kutotajwa majina walitiririka kwa kusema
kuwa ni kweli uongozi wa kundi hilo umetoa agizo watu wasishiriki
kutokana na tabia ya msanii huyo kutoshiriki katika misiba ya wasanii
wenzake.
“Ni kweli hilo lipo na lina ukweli
kwa njia moja au nyingine Wema bwana huwa hashiriki katika misiba ya
wasanii wenzake, kuna mtu muhimu sana na ana sauti katika kundi la Bongo
Movie amesema kuwa katika misiba iliyotokea ameshiriki misiba miwili
tu, wa marehemu Sharo na Kanumba kwa sababu alikuwa mtu wake,”anasema
kijana huyo.
Hili si jambo la kulifurahia kwa
wasanii kwani halijengi bali linaleta mgawanyiko wa moja kwa moja,
msanii mwingine alikiri kuwa Wema anabagua kushiriki misiba kwani wakati
amefariki marehemu John Maganga alipigiwa simu ili ashiriki katika
msiba lakini alisema yupo Location, hivyo wasanii wenzake wanamtenga ili
aone umuhimu wa kushiriki misiba ya wenzake.
Jana jioni nyumbani hakukuwa na
wasanii zaidi ya mtangazaji wa kipindi cha Take One Zamaradi Mketema
akiwa na Rais wa shirikisho la wasanii Simon Mwakifwamba na waombolezaji
wengine, huku baadhi ya wasanii wakifika pale na kuondoka jambo ambalo
Wema alilitafsiri kama walifika pale kutoa lawama ili asiwaone kama
hawajafika lakini hawakuwa na dhamira ya kweli mioyoni mwao.
No comments:
Post a Comment