Friday, November 8, 2013

SIRI IMEFICHUKA..!! KUMBE ZITIO KABWA NI KIBARAKA WA CCM, TAZAMA MABILIONI ALIYOLIPYWA KWA LENGO LA KUIVUNJA NGUVU CHADEMA..!! ~ UMBEA WA MJINI

SIRI IMEFICHUKA..!! KUMBE ZITIO KABWE NI KIBARAKA WA CCM, TAZAMA MABILIONI ALIYOLIPYWA KWA LENGO LA KUIVUNJA NGUVU CHADEMA..!! ~ UMBEA WA MJINI

CHEZEA K/KOO WEYE.....ME NILIZANI GALAXY S4 KUMBE SABUNI DAH !!

Tuache tamaa jaman ukija k/koo kuwa makin coz utajua umejipatia sm kwa bei chee kumbe umeuziwa sabun so nenda dukan moja kwa moja na wala usinunue sm mkonon



 Chezea k/koo ww dogo kaja pupa kauziwa sababu

Chezea k/koo ww dogo kaoneshwa sm kar katoa elfu tisin kaweka mfukon kutoa tena kumbe kauziwa sababu so tuache tamaa

MULUGO SAID "HATUJAFUTA ALAMA SIFURI MATOKEO YA MITIHANI "

Dodoma.Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema Serikali haijafuta daraja sifuri katika matokeo ya mitihani taifa ya shule za sekondari na kwamba ilichokifanya ni

SHILOLE HAWEZI LUGHA YA KINGEREZA...CHEKI UCHAPIAJI ALIOUFANYA....Shiole wapi English wewe ???


Shilole aliamua kutandika yai kwenye Instagram, ili kuzipa uzito shukrani zake za dhati kwa muongozaji wa video yake ya ‘Nakomaa na Jiji’ itakayotoka Jumamosi hii, Nisher.
Bahati mbaya, yai lake lilivunjika mapema wakati lilipokuwa likiufikisha ujumbe huo na kuwafanya watu waligeuzie mjadala.
Kama tumekuacha kwa lugha hiyo, ni kwamba Shilole aliandika Kiingereza kilichokosewa sarufi aka Broken English.

Shilole aliandika: I did ever think I would do a nice video like this thank you alot to my director @nisherbybee.

Monday, November 4, 2013

USHAHIDI WA RISITI YA ZITTO KABWE KUWA BADO ALIKUWA ANACHUKUA POSHO MPAKA 2011 YAANIKWA MTANDAONI

Kwa mjibu wa stakabadhi hii...zitto alikuwa napokea sitting allowance hadi 2011,kinyume nan alivyo mjibu muheshimiwa lema kwamba ameacha kupokea sitting allowance tangu 2009 hata zile za vikao vya madiwani...tujadili.

BONGO MOVIE WAMTENGA WEMA MSIBA WA BABA YAKE.

KATIKA hali isiyotarajiwa katika wasanii wanaounda kundi la Bongo movie wamejikuta wakijitenga kushiriki msiba wa Baba mzazi wa msanii mwenzao Wema Isack Sepetu, baada ya kuundwa zengwe na mmoja wa watu wenye ushawishi katika kundi hilo, Wema akiongea

LOWASSA ANGURUMA BUNGENI...SOMA HAPA ALICHOSEMA....

Katika hali isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, ambaye huongea kwa nadra bungeni, Edward Lowassa leo amenguruma na kutaka taifa kuacha kuweka

VITA YA ZITTO KABWE NA GODBLESS LEMA WOTE WA CHADEMA YAFIKIA PABAYA

Zitto Kabwe
Godbless Lema

Vs












Vita vya maneno kati ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe imefika pabaya.

Vita hiyo ya maneno iliyoanzishwa na Lema katika kikao cha wabunge wiki iliyopita kwamba Zitto anafanya unafiki kukataa posho, jana iliingia katika hatua nyingine baada ya mwakilishi huyo wa Arusha kumshushia tuhuma Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kwamba anakataa posho za vikao bungeni, lakini anapokea posho nyingi kutoka mashirika mbalimbali ya kijamii nchini.

Lema aliweka tuhuma hizo kwenye Mtandao wa Jamii Forum huku akisema kuwa, suala hilo halihitaji vikao vya chama kulijadili isipokuwa vyombo vya habari na hususani mitandao ya kijamii kwani hata Zitto hutumia mitandao hiyo.

Katika hoja yake, Lema alisema kuwa Zitto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) anakataa posho ya Sh70,000 kwa kikao kimoja cha Bunge, lakini anapokea Sh700,000 mpaka Sh1,000,000 kwa kikao kimoja cha kamati yake na haswa vile vinavyoandaliwa na mifuko ya jamii.

Hata hivyo, zitto alikanusha shutuma hizo akimtaka Lema kutoa ushahidi kama kuna mjumbe yoyote wa kamati ya PAC anayepokea posho, huku akieleza kuwa hawezi kubishana na Mbunge huyo wa Arusha mjini kwani yeye Zitto ni kiongozi wake ndani ya Chadema.

“Naomba kutaja masilahi yangu katika hili, wabunge wa kawaida wakialikwa katika vikao hivyo huwa wanalipwa Sh500,000 kwa kikao kwa siku . Mimi nimewahi kuhudhuria vikao hivyo mara mbili na nikalipwa hivyo pamoja na chai na chakula cha mchana.” alisema Lema.

Lema alisema posho hizo za wabunge ni tofauti na zile za Mwenyekiti wa PAC kwani yeye pamoja na posho ya Sh700,000 mpaka Sh1,000,000 hupewa mafuta ya gari au tiketi ya ndege ya kumtoa alipo na kumrudisha na kukodiwa hoteli yenye hadhi ya nyota nne mpaka tano ambayo kwa siku gharama yake ni Dola za Marekani 100 mpaka 600 kwa siku .

Akijibu hoja hizo, Zitto alisema tangu siku nyingi alikwisha piga marufuku kwa PAC kupokea posho kutoka taasisi au mashirika yanayosimamiwa na kamati hiyo.

“Toka nimekuwa Mwenyekiti wa POAC (Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma) sio tu nilipiga marufuku posho bali pia niliwashitaki PCCB (Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa) wabunge wanaochukua posho kutoka kwa taasisi za Serikali,” alisema Zitto.

Alieleza baada ya hatua hiyo, wabunge walihojiwa na PCCB kuhusu jambo hilo mpaka aliyekuwa Spika wa Bunge wakati huo, Samuel Sitta alipoingilia kati na kuwatetea wabunge hao.

“Hiyo ilikuwa mwaka 2009 kabla hata Lema hajawa mbunge, wajumbe wa kamati ya PAC wanalipwa posho za vikao kama wabunge wengine, lakini mimi sichukui posho hizo za vikao,” alisema na kuongeza:.

“Sio tu PAC hata kwenye Baraza la Madiwani na Baraza la Mashauriano la Mkoa wa Kigoma na popote kule. Hata NGO (Mashirika yasiyo ya Kiserikali) zikinialika kwenye vikao vyao sichukui posho za vikao. Nafasi yoyote ninayoalikwa kama mbunge sichukui posho za vikao,” alisema Zitto.

Alisema mtu yeyote mwenye ushahidi wa yeye kuchukua posho za vikao popote pale auweke hadharani na atawajibika.

“Sio kuandika uzushi au maneno ambayo mtu yeyote anaweza kuandika. Mimi siwezi kubishana na Lema maana ni kiongozi wake katika chama. Natumaini kadiri anavyokaa kwenye uwanja huu wa siasa atabadilika na kukomaa zaidi,” alisema Zitto.

Kwenye hoja yake, Lema alisema kuwa Chadema walikuwa wanakataa posho na kupendekeza mishahara ipandishwe na posho zisizo za lazima ziondolewe ili kuondoa mwanya wa ubadhirifu wa fedha za umma.

“Huu ndio uliokuwa msimamo wetu kulikuwa na msingi mkuu ambao ungekuwa na faida kubwa kwa nchi na watu wake,” alisema Lema.

Lema alisema kwamba kabla msimamo huu haujawekwa hadharani na kutafsiriwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Zitto tayari alishatoka katika vyombo vya habari na kujipambanua kuwa yeye hataki posho na wala hatachukua posho.

Lema alisema kuwa, anaamini kuwa umaskini siyo uzalendo. “Sipendi umaskini, nachukia umaskini, pia sipendi kuona mafanikio yangu yanabaki kwangu tu huku wengine wakiteseka, lakini siwezi pia kukumbatia umaskini kwa lengo lakuthibitisha uzalendo wangu.

Najua watu wa jimbo langu wanataka maji , umeme na huduma bora za afya na mambo mengi yenye sura hii, lakini sitang’oa bomba la maji nyumbani kwangu kwa sababu jirani yangu hana maji ila nimtasaidia kwa kadiri nitakavyoweza na yeye aepukane na adha hiyo ya ukosefu wa maji,” alisema Lema .